Pata taarifa kuu
TENNIS-FRENCH OPEN

Serena Williams kukabiliana na Maria Sharapova kwenye Fainali ya Mashindano ya French Open siku ya Jumamosi

Fainali ya Mashindano ya French Open kwa upande wa wanawake itakayopigwa kesho Jijini Paris nchini Ufaransa inatarajiwa kuwakutanisha Serena Williams dhidi ya Maria Sharapova baada ya kushinda michezo yao ya nusu fainali.

Serena Williams akisalimiana na Maria Sharapova baada ya mchezo wao wa Miami Open kabla ya kukutana kwenye French Open
Serena Williams akisalimiana na Maria Sharapova baada ya mchezo wao wa Miami Open kabla ya kukutana kwenye French Open
Matangazo ya kibiashara

Serena anatinga kwenye fainali ya French Open akisaka taji lake la pili mfululizo la mashindano hayo huku akiwa na kumbukumbu nzuri ya kumfunga Sharapova kwenye mashindano ya Miami Open.

Mchezaji nambari moja kwa ubora wa tennis upande wa wanawake duniani Serena ametinga fainali ya French Opern baada ya kumchakaza Sara Errani kutoka Italia kwa seti mbili bila ya jibu.

Serena ambaye amepoteza seti moja pekee kwenye mashindano ya mwaka huu ya French Open ameshinda kwa matokeo ya 6-0 na 6-1 katika mchezo uliokuwa na upande mmoja zaidi.

Mchezaji huyo raia wa Marekani baada ya mchezo huo amesema kwa sasa anaelekeza nguvu zake kwenye mchezo wa fainali baada ya kushinda kwa wepesi kwenye mchezo wa nusu fainali.

Mpinzani wa Serena ambaye ni Sharapova naye alitinga kwenye fainali ya French Open baada ya kulazimika kupambana na hatimaye kupata ushindi huo kutokana na hasimu wake Victoria Azarenka kumpa wakati mgumu.

Mchezo huo wa nusu fainali baina ya Sharapova na Azarenka ulilazimika kusitishwa kwa muda baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha wachezaji hao kutumia muda huo kujipimzisha kabla ya kuendelea.

Sharapova alifanikiwa kuanza kwa ushindi kwenye seti ya kwanza ka 6-1 kabla ya Azarenka hajajidhatiti na kushinda seti ya pili kwa 2-6 na kufanya matokeo kuwa moja kwa moja lakini Sharapova akamalizia seti ya tatu kwa ushindi kwa 6-4.

Sharapova amekiri mchezo wa fainali hautakuwa rahisi lakini lengo lake ni kuhakikisha anatwa taji la French Open mwaka huu hivyo anajipanga vyema kuhakikisha lengo lake linatimia.

Mchezo wa Fainali ya French Open upande wa wanawake inatarajiwa kupigwa siku ya jumamosi kabla ya siku ya jumapili kuchezwa fainali ya wanaume na hatimaye mashindano ya mwaka huu kutamatika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.