Pata taarifa kuu
TENNIS-FRENCH OPEN

Maria Sharapova atakumbana na Victoria Azarenka kwenye Nusu Fainali ya French Open baada ya kushinda Robo Fainali

Mchezaji nambari mbili kwa ubora wa tennis duniani upande wa wanawake Maria Sharapova atakumbana na mchezaji nambari tatu kwa ubora Victoria Azarenka katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya mashindano ya French Open.

Mchezaji Tennis Maria Sharapova akishangilia baada ya kufuzu hatua ya nusu fainali kwa kumfunga Jelena Jankovic
Mchezaji Tennis Maria Sharapova akishangilia baada ya kufuzu hatua ya nusu fainali kwa kumfunga Jelena Jankovic
Matangazo ya kibiashara

Sharapova alilazimika kupigana kufa na kupona ili aweze kutinga hatua ya nusu fainali ili kumshinda Jelena Jankovic baada ya kufungwa seti ya kwanza kwa matokeo ya 0-6 yaliyomfanya ajipange vizuri.

Mchezaji huyo namba mbili kwa ubora wa tennis upande wa wanawake aliibuka na kufanya vizuri katika seti ya pili na kufanikiwa kushinda 6-4 kabla ya kushinda katika seti ya tatu kwa 6-3 na kumfanya ashinde kwa seti mbili kwa moja.

Jankovic alitoa upinzani mkali lakini juhudi zake zikagongwa mwamba kutokana na Sharapova kuonekana makini sana na kurudisha mipira iliyokuwa ikipingwa kwa ufundi na mpinzani wake.

Sharapova baada ya kukata tiketi ya nusu fainali ya French Open akawaambia wanahabari kwa sasa anaangalia mchezowake wa nusu fainali dhidi ya Azarenka ili kupata nafasi ya kutinga fainali.

Mpinzani wa Sharapova, Azarenka naye ametinga nusu fainali baada ya kumfunga Maria Kirilenko katika mchezo uliochezwa kwa seti mbili pekee kabla ya mchezo huo wa robo fainali kumalizika.

Azarenka alishinda mchezo huo wa robo fainali kwa kupata ushindi wa seti mbili mbele ya Kirilenko kwa matokeo ya 7-6 na 6-2 na kufanikiwa kuingia kifua mbele hatua ya nusu fainali ya French Open.

Mshindi wa Sharapova na Kirilenko anatarajiwa kucheza katika fainali ya French Open dhidi ya mshindi wa Serena Williams na Sara Errani itakayochezwa siku ya alhamisi na fainali itacheza siku ya jumamosi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.