Pata taarifa kuu
TENNIS-FRENCH OPEN

Serena Williams na Sara Errani wanatarajiwa kupambana kwenye Nusu Fainali ya French Open mwaka huu

Mchezaji nambari moja wa tennis duniani upande wa wanawake Serena Williams ametinga nusu fainalia ya Michuano ya French Open baada ya kumchakaza mpinzani wake Svetlana Kuznetsova.

Serena Williams akirudisha mpira katika mchezo wake wa robo fainali dhidi ya Svetlana Kuznetsova katika Mashindano ya French Open
Serena Williams akirudisha mpira katika mchezo wake wa robo fainali dhidi ya Svetlana Kuznetsova katika Mashindano ya French Open
Matangazo ya kibiashara

Serena ametinga hatua ya nusu fainali huku akipoteza seti moja kwa mara ya kwanza tangu aanze mashindano ya French Open huku akishinda seti nyingine mbili kitu ambacho kimemfanya kukaribia kutinga fainali.

Mchezaji huyo nambari moja upande wa wanawake alianza seti ya kwanza vizuri kwa kumfunga Kuznetsova kwa 6-1 kabla hajafungwa katika seti ya pili kwa 3-6 lakini akafanya vizuri katika seti ya tatu na kushinda kwa 6-3.

Serena baada ya kushinda mchezo huo wa robo fainali amewaambia wanahabari mchezo ulikuwa mgumu kwake na kumfanya achoke kutokana na kupata upinzani mkubwa ambao ulitolewa na Kuznetsova.

Mchezaji huyo nambari moja kwa sasa ameweka rekodi ya kuwa mwanamke wa pili raia wa Marekani kutinga hatua ya nusu fainali ya Mashindano ya French Open kwa mara ya nne mfululizo akifuata nyayo za Jennifer Capriati.

Serena amemsifu sana Kuznetsova kutokana na kucheza vizuri lakini kwa upande wake amesema amesema lengo lake la kutwaa taji la French Open bado lipo pale pale.

Mpinzani wa Serena kwenye nusu fainali Sara Errani naye amefanikiwa kutinga nusu fainali baada ya kushinda mchezo wa robo fainali dhidi ya Agnieszka Radwanska katika mchezo uliokuwa na upinzani mkali.

Sara ameshinda mchezo wake kwa seti mbili kwa bila kwa matokeo ya 6-4 na 7-6 kitu ambacho kimemfanya akae kwenye nafasi nzuri ya kuweza kutinga fainali ya French Open mwaka huu.

Sara amekiri kumekuwa na shinikizo kubwa wakati mchezo huo ukiendelea lakini anafurahi sana kuweza kutinga hatua ya nusu fainali ya French Open akiwa na kibarua cha kupambana na Serena.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.