Pata taarifa kuu
SOKA

Timu za soka za vijana chipukizi kutafuta ushindi wa kuwafikisha nusu fainali michuano ya Afrika

Timu za taifa za mchezo soka za Ghana, Algeria na Benin zenye wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 zinahitaji ushindi katika mechi zao za Ijumaa usiku kujihakikisha nafasi ya kufuzu katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Afrika baina ya chipukizi inayoendelea mjini Algers Algeria.

Matangazo ya kibiashara

Kundi la  A lina Mirsi, Ghana, Algeria na Benin na tayari Misri imefuzu katika hatua hiyo ya nusu fainali baada ya kushinda michuano miwili iliyopita katika kundi hilo.

Ghana wanahitaji kuifunga Algeria ili kusonga mbele na wenyeji hao watafuzu ikiwa wataishinda Ghana au kuomba kuwa Misri iifunge Benin.

Benin nayo inahitaji kuifunga Misri na kuomba kuwa Algeria iishinde Ghana.

Misri wanaongoza kundi hilo kwa alama 6, Ghana ni ya pili kwa alama 3 huku Algeria na Benin zikiwa na alama 1.

Tayari Mali imefuzu katika kundi B  na inaongoza kundi hilo kwa alama 6, Nigeria ni ya pili kwa alama 3 wakati Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Gabon zikiwa na alama moja.

Mechi za mwisho za kundi hili zitachezwa siku ya Jumamosi ambapo Nigeria itamenyana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huku Mali ikicheza na Gabon.

Nigeria wanahitaji ushindi dhidi ya DR Congo ili kufuzu katika hatua hiyo ya nusu fainali, huku DRC nayo ikihitaji kushinda mchuano huo na kuomba kuwa Mali iifunge Gabon, ambayo inahitaji kuishinda Mali ili kufuzu na inahitaji kupata magoli mawili dhidi ya DRC ikiwa itakuwa imeshinda mechi yao.

Mataifa yatakayofika katika awamu ya nusu fainali yatawakilisha bara la Afrika katika michuano ya kombe la dunia nchini Uturuki kati ya mwezi Juni na Julai mwaka huu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.