Pata taarifa kuu
AFCON 2013

Afrika Kusini yapata ushindi wa kwanza, leo ni Ghana na Mali, Niger na DR Congo

Hatimaye timu ya taifa ya Afrika Kusini Bafanabafana imefanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza kwenye mechi za kombe la mataifa ya Afrika baada ya kuifunga Angola kwa mabao 2-0.

Itumeleng Khune, mlinda mlango wa Afrika Kusini akishangilia ushindi iliyoupata timu yake siku ya Jumatano
Itumeleng Khune, mlinda mlango wa Afrika Kusini akishangilia ushindi iliyoupata timu yake siku ya Jumatano Reuters
Matangazo ya kibiashara

Katika mchezo huo ambao wenyeji Afrika Kusini waliingia uwanjani wakiwa kwenye shinikizo kubwa lakutakiwa kushinda mechi hiyo, waliuanza mchezo kwa kasi na kufanikiwa kupata bao katika kipindi cha kwanza likifungwa na Siyabonga Sangweni.

Kipindi cha pili wachezaji wa timu ya taifa ya Angola walirejea kwa kasi na kulisakaama lango la Bafananafana lakini juhudi zao hazikuzaa matunda kwani mchezaji Lehlohonolo Majoro alipeleka kilio tena kwa waangola baada ya kuipatia tmu yake bao la ushindi.

Mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo wachezaji wa Afrika Kusini walizunguka uwanja mzima kuwashukuru mashabiki kwa kujitokeza kwa uwingi na kuonesha kuwa na imani na timu yao kuliko ilivyokuwa hapo awali.

Katika mchezo mwingine timu ngeni kwenye michuano ya mwaka, timu ya taifa ya Cape Verde ambapo alimanusura ipate ushindi baada ya kupata bao la kuongoza kabla ya timu ya taifa ya Morocco haijafanikiwa kusawazisha.

Hadi mwisho wa mchezo huo timu hizo zilimaliza kwa sare ya bao moja kwa moja.

Afrika Kusini ndio inaongoza kundi hilo ikiwa na alama 4 ikifuatiwa na Cape Verde yenye alama 2, Morocco yenye alama 2 na Angola inayoshika mkia kwenye kundi A ikiwa na alama 1.

Hii leo timu ya taifa ya Ghana itakuwa na kibarua dhidi ya timu ya taifa ya Mali wakati Niger wao watakuwa wenyeji wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC.

Wachambuzi wa masuala ya soka wanaona kuwa mechi za leno ni ngumu kwa timu zote kwakuwa zinahitaji ushindi ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kusonga mbele.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.