Pata taarifa kuu
ZAMBIA

Zambia yajipanga kurudisha nyumbani ubingwa wa kombe la Mataifa ya Afrika

Mshindi wa tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika ya BBC Chris Katongo anatarajia kuongoza kikosi cha wachezaji ishirini na sita wa Zambia Wanachipolopolo katika kuwania kutetea ubingwa wao katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika AFCON itakayoanza kutimua vumbi mwezi january mwakani nchini Afrika Kusini.

trulyzambian.com
Matangazo ya kibiashara

Akitoa orodha ya wachezaji waliochaguliwa kuiwakilisha Zambia katika michuano hiyo, msemaji wa shirikisho la soka nchini humo Erick Mwanza amesema kocha wao Herve Renard anaamini kikosi hicho kitaibuka na ubingwa kwa mara nyingine tena.

Hatua hiyo inakuja siku chache tu baada ya mabingwa hao kutandikwa bao moja kwa bila na majirani zao Tanzania katika mechi ya kirafiki iliyopigwa mwishoni mwa juma.

Michuano ya AFCON itaanza tarehe 29 kwa wenyeji Afrika kusini kumenyana na Cape Verde katika uga wa FNB Johannesburg, na mtanange wa fainali utapigwa tarehe 10 mwezi februari.

Kundi la kwanza katika michuano hiyo linaundwa na wenyeji Afrika kusini, Zambia, Ghana na Cote d'Ivoire. Kundi la pili linaundwa na Mali, Tunisia, Angola na Nigeria. Kundi la tatu litakuwa na Algeria, Burkina Faso, Morocco na Niger. Wakati kundi la nne ni Togo, Cape Verde, DRCongo pamoja na Ethiopia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.