Pata taarifa kuu
CECAFA-UGANDA

Kilimanjaro Stars, Zanzibar zatinga nusu fainali, leo ni zamu ya Uganda, Ethiopia, Malawi na Kenya kuchuana kwenye robo fainali

Michuano ya kombe la Tusker Chalenji inayotimua vumbi nchini Uganda chini ya baraza la vyama vya soka Afrika Mashariki CECAFA imeendelea kwa timu mbili za awali kukata tiketi kucheza hatua ya nusu fainali.

Mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars John Boko akishangilia goli alilofunga jana dhidi ya Rwanda
Mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars John Boko akishangilia goli alilofunga jana dhidi ya Rwanda Kwa hisani ya Blog ya Issa Michuzi
Matangazo ya kibiashara

Timu za mwanzo kukata tiketi kucheza nusu fainali zilikuwa ni ile ya Tanzania "Kilimanjaro Stars" na ile ya Zanzibar "Zanzibar Hero".

Kilimanjaro Stars ilifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kufanikiwa kuchomoza na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya timu ya taifa ya Rwanda kwenye mchezo ambao umetoa matokeo ambayo hayakutarajiwa na wengi.

Magoli ya Kilimanjaro Stars yalifungwa na Amri Kiemba na John Boko ambaye sasa amefikisha idadi ya magoli 5 sawa na mshambuliaji mwenzake Mrisho Ngassa.

Timu nyingine ambayo ilifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ni Zanzibar Hero ambayo ilifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuishinda timu ya taifa ya Burundi kwa njia ya mikwaju ya Penalt.

Timu hizo zilimaliza dakika tisini bila kufungana na hivyo kuingia kwenye hatua ya matuta na kushuhudia Zanzibar ikipata ushindi wa penalt 6 -5 dhidi ya Burundi.

Hii leo kuna mechi nyingine za robo fainali ambapo timu ya taifa ya kenya harambee Star itakuwa na kibarua dhidi ya Malawi the Flames kwenye mchezo ambao unatarajiwa kuwa mgumu kwa pande zote mbili.

Mtanange mwingine ni ule wa wenyeji timu ya taifa ya Uganda ambayo itakuwa na kibarua dhidi ya Ethiopia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.