Pata taarifa kuu
UGANDA

Zanzibar Heroes yaibamiza Rwanda, uwanja wawa kikwazo kwa timu zote

Kindumbwendumbwe cha mashindano ya CECAFA Chalenji kiliendelea tena hii leo huku Zanzibar ikishuka dimbani kukabiliana na Rwanda katika mchezo wa pili.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Katika mchezo wa pili katika uwanja wa Namboole nchini Uganda ilipambana vikali dhidi ya Rwanda na hatimaye kuidabisha Rwanda kwa mabao 2-1 katika uwanja ambao wachezaji walitota kwa tope kama samaki aina ya kambale kutokana na mvua kubwa kunyesha.

Matokeo hayo yanalifanya kundi hilo kutotabirika kwa timu zitalazimika kusubiri mechi za mwisho.

Mchezo wa kwanza wenyewe uliikutanisha Malawi na Eritrea huku Eritrea ikiionyesha upinzani mkali tofauti na ilivyotarajiwa.

Katika mchezo huo Malawi wameandikisha ushindi wake wa kwanza katika michuano inayoendeela jijini Kampala Uganda baada ya kuishinda Eritrea mabao 3 kwa 2 katika mchuano mgumu uliochezwa Alhamsihi jioni katika uwanja wa Naambole.

Mchuano huo ulichezwa katika mazingira magumu kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha na kusababisha uwanja kujaa maji.

Makocha pamoja na wachezaji wamelalamikia hali hiyo na hata kudai kuwa gali hiyo imechangia wao kupata wakati mgumu uwanjani kama ilivyoshuhudiwa katika mchunaon nwa Jumatano kati ya Burundi na Tanzania Bara.

Katika hatua nyingine viongozi wa CECAFA wamekerwa na idadi ndogo ya mashabiki wanaokuja kushuhdia michunai hiyo na wameamua kuwa hakutakuwa na kiingilio katika michuano yote ya makundi itakayokamalika Jumamosi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.