Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Luis Suarez afurahia kuendelea kubaki Liverpool

Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez ameweka bayana kuwa anafurahia uwepo wake katika klabu hiyo na anapenda kuendelea kusalia hapo kwa miaka mingi zaidi kadri inavyowezekana.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya Suarez inakuja kufuatia tetesi zilizokuwa zimesagaa kuwa mshambuliaji huyo huenda akaihama klabu yake ya sasa na kujiunga na Manchester City.

Suarez mwenue umri wa miaka 25 amesema kuwa licha ya furaha aliyonayo katika klabu ya Liverpool pia anavutiwa na utendaji kazi wa Meneja Brendan Rodgers kwa jinsi anavyoratibu mambo kwenye klabu hiyo bora katika ulimwengu wa soka.

Aidha Suarez ameweka bayana kuwa kikosi hicho kina mshikamano wa hali ya juu kwani licha ya kutopata matokeo mazuri bado wana umoja na wanatumaini ya kujiboresha zaidi ili waendelee kung'ara katika mchezo wa kandanda ulimwenguni.

Kwa upande wake Meneja Rodgers ameweka bayana kuwa hatakubali kumwachia mshambuliaji huyo ambaye alijiunga kikosini hapo mwaka 2011 akitokea Ajax na ameweka rekodi nzuri kwa kufunga magoli 17 katika mechi 39 alizoshuka dimbani katika muda alioictumikia Liverpool.

 

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.