Pata taarifa kuu
ZAMBIA-AFRIKA KUSINI

Kocha Mkuu wa Zambia Renard ataja Kikosi kitakachoshuka dimbani kupambana na Bafana Bafana

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Zambia Herve Renard ametaja Kikosi chake cha wachezaji ishrini na wanne ambacho kitashuka Dimbani kucheza mchezo wa kirafiki na Afrika Kusini tarehe 14 Novemba kwenye Jiji la Johannesburg.

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zambia Chipolopolo wakishangilia Ubingwa waliopata wa Kombe la Mataifa ya Afrika huko Gabon
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zambia Chipolopolo wakishangilia Ubingwa waliopata wa Kombe la Mataifa ya Afrika huko Gabon Reuters
Matangazo ya kibiashara

Renard kwenye kikosi hicho amewajumuisha wachezaji kadhaa ambao aliwaweka kando hapo awali akiwemo Mshambuliaji Collins Mbesuma anayecheza Ligi Kuu nchini Afrika Kusini kunako Klabu ya Orlando Pirates.

Mbesuma aliwekwa kando kwenye kikosi ambacho kilikuwa kinasaka tiketi ya kushiriki kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013 nchini Afrika Kusini ambapo Zambia waliwaondosha Uganda kwa mikwaju ya penalti.

Kikosi cha Kocha Renard kimejumuisha chipukizi kadhaa wakiwemo Mukuka Mulenga anayecheza Power Dynamos, Shadreck Malambo anayesakata kabumbu Zanaco pamoja na Jacob Mulenga kutoka Klabu FC Utrecht ya Uholanzi.

Msemaji wa Chama Cha Soka nchini Zambia Erick Mwanza amesema mchezo huo ni muhimu kwao ikiwa ni maandalizi ya kutetea Ubingwa wa Komba la mataifa ya Afrika ambao waliutwaa mapema mwaka huu.

Mchezaji wa TP Mazembe Rainford Kalaba ambaye ni majeruhi ameachwa kwenye kikosi hicho kutokana na yeye hadi saa hii kushindwa kuanza mazoezi tangu aumie kwenye mchezo wa Kombe la Ligi ya Mabigwa tarehe 6 Oktoba.

Zambia imeweka kwenye Kundi C kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ambayo yatafanyika mwakani mwezi Juni na itapambana na Nigeria, Ethiopia na Burkina Faso.

Kikosi kamili cha wachezaji ambao wameitwa na Timu wanazocheza ni: Kennedy Mweene (Free State Stars, RSA), Danny Munyau (Red Arrows), Joshua Titima (Power Dynamos), Emmanuel Mbola (FC Porto, Portugal), Joseph Musonda (Golden Arrows, RSA), Davies Nkausu (SuperSport United, RSA), Chintu Kampamba (Unattached), Stoppila Sunzu (TP Mazembe, DRC), Hichani Himoonde (TP Mazembe, DRC), Nathan Sinkala (TP Mazembe, DRC), William Njobvu (Hapoel Be'er Sheva, Israel), Noah Chivuta (Free State Stars, RSA), Isaac Chansa (Henan Jienye, China), Mukuka Mulenga (Power Dynamos), Rainford Kalaba (TP Mazembe, DRC), Chisamba Lungu (FC Urals, Russia), Shadreck Malambo (Zanaco), Felix Katongo (Primero de Agosto, Angola), Jonas Sakuwaha (El Merreikh, Sudan), James Chamanga (Dalian Shide, China), Collins Mbesuma (Orlando Pirates, RSA), Chris Katongo (Henan Jienye, China), Emmanuel Mayuka (Southampton, England), Jacob Mulenga (FC Utrecht, Holland).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.