Pata taarifa kuu
Uganda- Zambia

Mbivu na mbichi kujulikana leo kati ya “The Cranes” na “Chipolopolo”

Timu ya taifa ya soka ya Uganda “The Cranes” leo inaingia dimbani kuvaana na timu ya taifa ya Zambia “Chipolopolo” kuwania kufuzu kushiriki fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2013 zitakazo fanyika nchini Afrika Kusini. 

Kikosi cha timu ya taifa ya Uganda "The Cranes"
Kikosi cha timu ya taifa ya Uganda "The Cranes" ukzambians.co.uk
Matangazo ya kibiashara

Golikipa namba moja wa timu ya taifa ya soka ya Uganda Dennis Onyango amesema kitendo cha timu yake kufungwa bao moja kwa bila na timu ya taifa ya Zambia, Chipolopolo katika mchezo wa awali kinaiweka katika hali ngumu The Cranes.

Hata hivyo golikipa huyo amesema hakuna haja ya kukata tamaa bali The Cranes inatakiwa kucheza mchezo wa kushambulia ili iweze kupata ushindi katika mchezo huo wa marudiano utakaofanyika nchini Uganda.

Endapo The Cranes itafungwa ama kutoka sare ya aina yoyote itakuwa imezamisha matumaini ya kufuzu kucheza fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2013 nchini Afrika Kusini.

Aidha Onyango amesema kuwa ushindi na hatimaye kufuzu kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1978 kwa The Cranes vinaweza kuwa zawadi ya miaka 50 ya uhuru wa Uganda na wananchi wake.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.