Pata taarifa kuu
Uingereza

Rooney apania kuipaisha Uingereza fainali za Kombe la Dunia 2014

Nguli wa kimataifa katika soka nchini Uingereza Wayne Rooney anayeitumikia klabu ya Manchester United anatarajiwa kuongoza kikosi cha England dhidi ya San Marino katika mechi za kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia zitakazofanyika nchini Brazil mwaka 2014.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Rooney mwenye umri wa miaka 26 ameteuliwa na kuongoza kikosi hicho baaada ya nahodha mkuu Steven Gerald kusimamishwa katika michezo kadhaa na nahodha msaidizi Frank Lampard kutoweza kushuka dimbani kutokana na majeraha yanayomkabili.

Rooney amewaahidi wachezaji wenzake na mashabiki wake kuwa hatorudia makosa yaliyokwamisha jitihada zake katika fainali za EURO kwa mwaka 2012 baada ya kupata adhabu iliyomsababisha kutoshuka dimbani katika mechi mbili mfululizo za kimataifa.

Mshambuliaji huyo alikosa mechi kati ya Ufaransa na Sweden baada ya kupewa kadi nyekundu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.