Pata taarifa kuu
UGANDA-ZAMBIA

The Cranes na Chipolopolo hapatoshi kesho mbio za kuelekea Afrika Kusini 2013

Mchezo kati ya timu ya taifa ya Zambia, Chipolopolo na timu ya taifa ya soka ya Uganda utapigwa kesho jumamosi na endapo The Cranes itafungwa ama kutoka sare ya aina yoyote itakuwa imepoteza nafasi ya kufuzu kucheza fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2013 nchini Afrika Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo wachezaji wa timu hiyo wametakiwa kutokakata tamaa na kutakiwa kucheza mchezo wa kushambulia ili waweze kupata ushindi katika mchezo huo wa marudiano utakaofanyika hiyo kesho katika uwanja wa Namboole jijini Kampala.

Matumaini ya Uganda kuiwakilisha vyema Afrika mashariki yaliingia doa ambalo linapaswa kusafishwa baada ya kukubali kipigo cha 1-0 kutoka kwa Chipolopolo katika mchezo wa awali uliofanyika nchini Zambia.

The Cranes inaweza kushinda mchezo huo kama Chipolopolo itacheza kwa kujihami zaidi hali ambayo inaweza kuipa nafasi Uganda.

Zambia itashuka dimbani ikiwa imeweka mkakati wa kulinda goli lake hivyo Cranes wakishambulia zaidi wanaweza kupata ushindi katika mchezo huo muhimu kwa timu zote mbili.

The Cranes inalazimika kujilinda ili kuzuia washambuliaji wa Chipolopolo kupenya katika ngome yao kirahisi na kupata mabao.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.