Pata taarifa kuu
Ghana-Malawi

Timu ya taifa ya Ghana yapiga kambi Nairobi kabla ya kupambana na Malawi

Timu ya taifa ya Ghana ya soka imepiga kambi nchini Kenya kabla ya mchezo wake wa pili na timu ya taifa ya Malawi wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zinazotarajiwa kufanyika nchini Afrika Kusini mwaka 2013.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Mchezo huo wa marudiano unatarajiwa kupigwa Oktoba 13 na timu ya Ghana maarufu kama Black Stars imesili leo asubuhi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta kwa ajili ya kambi hiyo.

Kocha wa timu hiyo Kwasi Appiah na msaidizi wake Maxwell Konadu wanatarajiwa kuungana na timu hiyo muda mfupi ujao na timu hiyo imeahidi kufanya maajabu ili kujipatia mafanikio.

Timu hiyo inajumuishwa na wachezaji mbalimbali, huku upande wa walinda mlango ukiwakilishwa na Adam Kwarasey (Stromgodset, Norway), Philemon McCarthy (Hearts of Oak), Fatau Dauda (AshantiGold).

Upande wa ulinzi ni John Paintsil (Hapoel Tel Aviv, Israel), Harrison Afful (Esperance, Tunisia), David Addy (Vitoria Guimaraes, Portugal), John Boye (Rennes, France), Isaac Vorsah (Red Bull Salzburg, Austria), Jonathan Mensah (Evian Thonon Gaillard, France).

Viuongo ni Anthony Annan (Osasuna, Spain), Daniel Nii Adjei (Asante Kotoko), Mubarak Wakaso (Espanyol, Spain), Emmanuel Agyemang Badu (Udinese, Italy), Kwadwo Asamoah (Juventus, Italy), Christian Atsu (Porto, Portugal), Solomon Asante (Berekum Chelsea), Andre Ayew (Marseille, France), Rabiu Mohammed (Evian, France).

Safu ya ushambuliaji inawajumuisha wachezaji Emmanuel Clottey (Esperance, Tunisia), Abdul Majeed Warris (Hacken, Sweden), Asamoah Gyan (Al Ain, UAE).

The Black Stars wanatarajiwa kuondoka Nairobi kuelekea Lilongwe nchini Malawi siku ya Ijumaa kabla ya mchezo wao wa Jumamosi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.