Pata taarifa kuu
Cricket

Pakistan yaondolewa katika michuani ya Cricket ya Twenty20

Nahodha wa timu ya taifa ya Pakistan ya mchezo wa Cricket Mohammad Hafeez amesema licha ya nchi hiyo kuondolewa katika mashindano ya dunia ya Twenty20 na wenyeji Sri Lanka, kikosi chake kilionesha mchezo wa hali ya juu. 

Matangazo ya kibiashara

Aidha Hafeez ameongeza kuwa Sri Lanka ilicheza vema zaidi na inastahili kufika fainali baada ya kuwashinda kwa alama 139.

Hii ni nusu fainali ya pili kwa Pakistan kushindwa baada ya kufungwa tena mwaka 2010 wakati wa michezo hii na Australia wakati michuano hiyo ilipoandaliwa nchini West Indies.

Mashindano hayo ya Twenty20 yalizinduliwa mwaka 2007 nchini Afrika Kusini walipomaliza wa pili na baadaye kunyakua ubingwa wa taji hili mwaka 2009.

Fainali ya makala ya mwaka huu itachezwa siku ya Jumapili kati ya wenyeji Sri Lanka na Australia au West Indies ambao wanacheza nusu fainali ya pili baadaye siku ya Ijumaa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.