Pata taarifa kuu
michezo

Drogber na Anelka huenda wakauzwa na klabu ya Shanghai 'Shenhua

Hatima ya Wacheza kandanda nyota kutoka klabu ya Chelsea Didier Drogba na Nicolas Anelka ambao wanachezea klabu ya Shanghai Shenshua huenda ikatumbukia nyongo na wakawa wamecheza mechi ya mwisho kwa klabu ya hiyo ya Shenhua, taarifa zimebainisha jumatano.

Wachezaji wa kandanda wa kimataifa Nicolas Anelka na Didier Drogber wanaochezea klabu ya Shanghai Shenhua
Wachezaji wa kandanda wa kimataifa Nicolas Anelka na Didier Drogber wanaochezea klabu ya Shanghai Shenhua Maltastar.com
Matangazo ya kibiashara

Taarifa zimebainisha kuwa mkuu wa klabu ya Shenhua,bilionea Zhu Jun ametishia kusitisha malipo ya wachezaji hao wa kimataifa kufuatia mgogoro uliopo baina ya wanahisa.

Mmoja kati ya viongozi wa klabu hiyo amenukuliwa akisema kama Zhu Jun hatoweza kuungwa mkono na wanahisa wengine atakachofanya ni kuwalipa wachezaji hao kwa kadri aonavyo yeye.

Kiongozi huyo alikaririwa akisema kuwa bado haijulikani kama Drogber atacheza mechi itakayofanyika September 15 au la,jambo ambalo limezua maswali na kuwashangaza wadau na mashabiki wa kandanda ulimwenguni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.