Pata taarifa kuu
SOKA

Sare na ushindi zatawala mechi za soka za kirafiki

Taifa Stars ya Tanzania ilitoka sare ya mabao 3 kwa 3 na Bostwana katika mchuano wa kimataifa wa kirafiki Jumatano usiku katika uwanja wa kimataifa wa Molepolole jijini Gaborone.

Matangazo ya kibiashara

Mwinyi Kazimoto alifungua safu ya mabao katika mechi hiyo baada ya kuipa Taifa Stars bao la kwanza katika dakika za mwanzo mwanzo za mchuano huo kabla ya Erasto Nyoni kuipa Taifa Stars bao la pili.

The Zebras ya Bostwana ilitoka nyuma na kusawazisha mabao hayo na kufunga bao la ushindi na baadaye Mrisho Ngassa kuifungia Tanzania bao la kusawazisha katika mechi hiyo iliyokamilika kwa mabao 3 kwa 3.

Sare nyingine pia ilishuhudiwa kati ya Cote Dvoire na Urusi mchuano uliochezwa mjini Moscow.

Urusi ilipata bao lake la kwanza kupitia kwa mshambulizi wake Alan Dzagoev katika dakika ya 55 ya mchezo huo kabla ya mchezaji wa Cote Dvoire Max Gradel kuisawazishia timu yake.

Urusi ilitawala mechi hiyo ambayo ilikuwa na wachezaji wa kimataifa wa cote Dvoire kama vile Salomon Kalou, Kolo Toure na Didier Drogba .

Argentina nayo iliishinda Ujerumani mabao 3 kwa 1 huku, Ubelgiji ikiishinda Uholanzi mabao 4 kwa 2.

Mataifa mengi yalitumia mechi hizo kwa maandalizi ya mechi za kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil, huku mataifa ya Afrika yakijiandaa kwa michuano ya kufuzu kwa kombe la mataifa ya Afrika mwaka ujao nchini Afrika Kusini.

Uhispani iliicharaza Puerto Rico mabao 2 kwa 1 kupitia wachezaji wake Santi Cazorla na Cesc Fabregas, huku Uingereza ikiishinda Italia kwa mabao 2 kwa 1.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.