Pata taarifa kuu
AFON 2013

Zambia ,Ghana na Cote Dvoire mechi za kirafiki-Soka

Timu ya taifa ya soka ya Zambia itamenyana na Korea Kusini, Black Stars ya Ghana itakuwa China na Cote Dvoire nchini Urusi katika mechi za kirafiki Jumatano hii kujiandaa kwa mechi za kufuzu kwa kombe la mataifa bingwa barani Afrika itakayoandaliwa mwaka ujao nchini Afrika Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Chipolopolo ndio mabingwa watetezi wa taji hilo na wachezaji sita walioshiriki katika fainali mapema mwaka huu nchini Gabon na Equitorial Guinea kipa Kennedy Mweene, mlinzi Davies Nkausu, viungo wa kati Chisamba Lungu, Isaac Chansa na washambulizi Christopher Katongo na Emmanuel Mayuka watashiriki katika mchuano huo mjini Seoul.

Wiki iliyopita, Zambia iliishinda Zimbabwe mabao 2 kwa 1 katika mchuano mwingine wa kirafiki na itakutana na Uganda katiak mechi ya kufuzu kwa fainali hiyo.

Mshambulizi wa Black Stars ya Ghana Asamoah Gyan anayecheza soka ya kulipwa katika nchi za Mmiliki za kiarabu amejumishwa tena katika kikosi cha kocha Kwesi Appiah baada ya kutangaza mapema mwaka huu kuwa alikuwa amestaafu kuichezea timu ya taifa.

Nayo Cote Dvoire ambayo itakuwa inacheza na Senegal katika mechi mbili za kufuzu, itakuwa na wachezaji 24 kumenyana na Urusi katika mchuano huo wa kirafiki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.