Pata taarifa kuu
LONDON OLIMPIKI 2012

Nusu fainali ya Olympic mpira wa miguu kwa upande wa wanaume kuchezwa leo

Nusu fainali ya mpira wa miguu kwa upande wa wanaume kwenye michuano ya olympic inatarajiwa kutimua vumbi hii leo kwa miamba ya soka barani Ulaya na Amerika kushuka viwanjani.

Marta mchezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Brazil ambayo imeaga mashindano
Marta mchezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Brazil ambayo imeaga mashindano Reuters
Matangazo ya kibiashara

Katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza timu ya taifa ya Mexico wao watakuwa wenyeji wa timu ya taifa ya Japan kwenye mchezo ambao unabashiriwa kuwa utakuwa mgumu kwa pande zote mbili hasa kutokana na aina ya mchezo ambao timu hizi zinacheza.

Hata hivyo timu ya taifa ya Japan inapewa nafasi kubwa ya kuweza kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa hii leo kutokana na michezo yake ya kufuzu kufika hatua hiyo kupata mafanikio makubwa kwani haikupoteza mchezo hata mmoja.

Kwa upande wake timu ya taifa ya Mexico inajivunia kuweza kutinga hatua hiyo baada ya kuwaondoa vijana wagumu wa Senegal kwenye mchezo uliokuwa mgumu na wakusisimua.

Kwenye nusu fainali nyingine itazikutanisha timu za taifa za Korea Kusini ambayo itakuwa mwenyeji wa timu ya taifa ya Brazi kwenye mchezo mwingine ambao nao unatarajiwa kuwa mgumu kwa timu zote mbili.

Kwa upande wa wanawake timu ya taifa ya Ufaransa hapo jana iliangukia pua baada ya kuambulia kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Japan wakati timu ya wanawake ya Canada iliambulia kipigo cha mabao 4-3 dhidi ya Ufaransa.

Kwa matokeo hayo, Ufaransa na Canada watacheza mchezo wao siku ya alhamisi kuwania medali ya fedha wakati Japan na Marekani watacheza kuwania medali ya Dhahabu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.