Pata taarifa kuu
DRC

TP Mazembe yaivuta shati Berekum Chelsea

Klabu ya Berekum Chelsea ya Ghana ililazimisha sare ya mabao 2 kwa 2 na TP Mazembe ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo mjini Lubumbashi katika mechi za kundi la pili za kutafutwa ubingwa wa klabu bora barani Afrika mwishoni mwa juma lililopita.

Matangazo ya kibiashara

TP Mazembe ilikuwa ya kwanza kupata bao lake kupitia kwa mshambulizi Tresor Mputu katika dakika ya 11 na ya 32 katika kipindi cha kwanza cha mchuano huo.

Katika kipindi cha pili Berekum Chelsea ilitoka nyuma na kusawazisha kupitia mkwaju wa penalti bao lililofungwa na Emmanuel Clottey katika dakika ya 71 kabla ya Clottey kusawazisha katika dakika ya 84 kwa kufunga bao la pili.

Nayo Al Ahly waliifunga watani wao wajadi Zamalek bao 1 kwa 0 mjini cairo katika mchuano ambayo uklichezwa bila ya mashabiki kutokana na sabbau za kiusalama.

Shirikisho la soka nchini humo limepiga marufuku mashabiki kuhudhuria michuano yeoete ya sokja ya kimataifa na kusimamaisha ligi kuu ya soka nchini humo kwa miaka miwli baad aya kuuawa kwa mashabii zaiid ya 70 mapema mwaka huu mjini Port Said baad aya kuzuka kwa makabiliano kati ya mashabiki wa Al-Masry na Al -Ahly.

Etoile Sahel ya Tunisia iliytoka sare ya kutofungana na Sunshine Stars ya Nigeria mjini Tunis,huku mshambuliz wa Cameroon Yannick Ndjeng akiwapa ushindi mabingwa watatetezi Esperance ya Tunisia wa mabao 3 kwa 2 dhidi ya ASO Chlef kutoka Algeria .

Mechi za marudiano zitachezwa mapema mwezi ujao.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.