Pata taarifa kuu
Michezo-Kombe la Dunia 2014

Tanzania na DRCongo zajiweka kwenye nafasi nzuri kuelekea Brazil 2014, huku Cameroon ikilazwa na Libya.

Katika mashindano ya kufuzu kuelekea kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil, yalioshuhudiwa jana Jumapili katika viwanja mbalimbali barani Afrika, timu ya taifa ya Tanzania  'Taifa Stars' imeilambisha mchanga Gambia kwa kuilaza mabao 2-1 katika mchezo ulipoigwa kwenye uwanja wa Tifa jijini Dar Es Salaam.

Mashabiki wa timu ya taifa ya Tanzania
Mashabiki wa timu ya taifa ya Tanzania RFI
Matangazo ya kibiashara

Katika mchezo huo Stars walilazimika kusawazisha kabla ya kupata ushindi huo muhimu katika harakati zake za kuwania kufuzu kushiriki Fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.

Kwa matokeo hayo Tanzania sasa inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi tatu na ikiwa pointi moja nyuma ya vinara Ivory Coast yenye pointi nne baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Morocco inayoshika nafasi ya pili na Gambia inashika mkia ikiwa na pointi mbili.

Wakati huo huo timu ya taifa ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo"Leopards" waliilaza Togo kwa mabao 2-0. Wachezaji wa DRCongo walicheza wakiwa nusu baada ya mchezaji wao kupewa kadi nyekundu.

Timu ya taifa ya Mali, iliishinda Algeria mabao 2-1, huku Guinea ikilazimishwa kichapo cha mabao 3-1. Timu ya taifa ya Libya ikailazimisha Cameroon mabao 2-1, huku Liberia ikitoka sare ya kutofungana na Angola.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.