Pata taarifa kuu
TENNIS

Djokovic na Nadal wasonga mbele michuano ya Monte Carlo

Michuano ya Tenesi ya Monte Carlo inayoendelea katika jiji la Monaco nchini Ufaransa imeendelea kushika kasi, huku wachezaji wawili Novak Djokovic na Rafael Nadal wakifanikiwa kusonga mbele. 

Novak Djokovic mchezaji nambari moja wa mchezo wa Tennesi
Novak Djokovic mchezaji nambari moja wa mchezo wa Tennesi Reuters
Matangazo ya kibiashara

Michuano hiyo ambayo inashirikisha magwiji kadhaa tenesi duniani umeshuhudia bingwa nambari moja wa mchezo huo Novak Djokovic akifanikiwa kusonga mbele kwenye hatua inayofuata baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya Andreas Seppi.

Katika mchezo huo Djokovic alifanikiwa kupata ushindi wa seti mbili bila kwa matokeo ya 6-1 na 6-4.

Katika mchezo mwingine mchezaji Rafael Nadal alifanikiwa kusonga mbele kwenye hatua inayofuata ya michuano hiyo baada ya kufanikiwa kumfunga Jarkko Nieminen kwa seti mbili bila kwa matokeo ya 6-3 na 6-4.

Tomas Berdych alifanikiwa kuibuka na ushindi wa seti mbili bila kwa matokeo ya 7-6 na 6-1.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.