Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Kocha wa Manchester United Ferguson akiri mbio za Ubingwa kati yao na Manchester City bado zinaendelea

Kocha Mkuu wa Klabu ya Manchester United Sir Alex Ferguson anaamini mbio za Ubingwa wa Ligu Kuu nchini Uingereza bado zinapamba moto licha ya mpinzani wake Mkuu Roberto Mancini ambaye anainoa Manchester City kusema United ndiyo mabingwa msimu huu.

Kocha Mkuu wa Manchester United Sir Alex Ferguson
Kocha Mkuu wa Manchester United Sir Alex Ferguson
Matangazo ya kibiashara

Ferguson amesema kauli ya Mancini imekuja mapema sana wakati huu ambapo kila timu imesalia na michezo mitano kabla ya bingwa mpya hajatambulika licha ya mpambano kuwa katika ya Manchester United na City.

Kocha huyo mkongwe wa Klabu ya Manchester United amesema timu hizo mbili zote zina nafasi ya kutwa ubingwa katika michezo hiyo mitano ambayo inakusanya jumla ya pointi kumi na tano.

Kauli ya Ferguson imekuja baada ya Mancini kuwaambia wanahabari mbio za ubingwa zimeshafikia mwisho licha ya Manchester United kufungwa dhidi ya Wigan Athletic huku City wakishinda mbele ya West Brom na kupunguza tofauti ya pointi na kusalia tano.

Ferguson amepuuza kauli hiyo huku akitolea mifano kadhaa ambayo imeshatokea kwenye Ligi Kuu Nchini Uingereza katika miaka iliyopita wakati mbizo za ubingwa zikiwa katika mwelekeo kama huu.

Kocha huyo wa Manchester United ameenda mbali zaidi na kusema hata City walianza vyema ligi na kuweza kujikusanyia pointi nyingi lakini walivyotetereka ndiyo wakatoa nafasi kwa klabu yake kuweza kuchukua usukani wa ligi.

Ferguson amesema kitu muhimu kwa wachezaji wake kwa sasa ni kuendelea kupambana na kuhakikisha wanashinda michezo yao miwili inayofuata ambayo watacheza nyumbani Old Trafford.

Katika hatua nyingine Ferguson amesema Kiungo mkongwe wa Klabu hiyo ambaye alistaafu kucheza soka Paul Scholes yupo tayari kurejea uwanjani kwenye mchezo dhidi ya Aston Villa akiamini ataongeza nguvu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.