Pata taarifa kuu
Ligi kuu Uingereza

Hali ya afya ya mchezaji wa Bolton Fabrice Mwamba yaendelea kuimarika

Ma Dactari wa Hospitali ya Chest Hospital nchini Uingereza wamethibitisha kuwa hali ya Afya ya mchezaji Fabrice Mwamba wa timu ya Bolton alieanguka uwanjani siku nane zilizopita yaendelea kuimarika.

Fabrice Mwamba
Fabrice Mwamba
Matangazo ya kibiashara

Weekand hii mchezaji huyo aliondoka kitandani pekeake, na kuangalia runinga na kuanza kula, hata hivyo yupo chini ya uangaliz mkubwa wa madactari wa hospitali ya London Chest Hospital.

Kocha wa Bolton alifahamisha kuwa Mwamba aliangalia jana jumapili vipande vya mechi ya timu yake iliposhinda mabao 2-1 dhidi ya Blackburn katika ligi kuu ya Uingereza. Kocha wa Bolton amesema kwamba Mwamba alisinzia wakati timu hiyo ilikuwa inaongoza mabao mawili kwa bila, haijulikani iwapo anafahamu matokeo ya mwisho. Hata hivyo hali yake sio mbaya, alifahamisha kocha wa Bolton.

Fabrice Mwamba raia wa Uingereza mwenye asili ya DRCongo mwenye umri wa miaka 23 alianguka uwanjani Machi 17 mwaka huu wakati timu yake ilikuwa ikipepetana na Tottenham kwenye uwanja wa White Hart Lane jijini London, mapigo ya moyo yalisimama kwa muda wa dakika 78.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.