Pata taarifa kuu
Uingereza

Manchester City kutafuta uongozi wa ligi ya soka nchini Uingereza

Manchester City inacheza na Chelsea katika mechi ya soka ya  klabu bingwa nchini Uingereza Jumatano usiku, mchuano ambao unaangaziwa utaamua ikiwa Manchster City watakuwa katika nafasi bora ya kushinda taji la msimu huu na pia ikiwa watakuwa katika harakati zao za kutafuta kurejea katika uongozi wa ligi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Manchester City wanacheza wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Etihad wakiwa katika nafasi ya pili alama nne nyuma ya Manchester United ambayo inaongoza msururu wa ligi hiyo kwa alama 70.

Chelsea ambayo iko katika nafasi ya tano kwa alama 49 nayo itakuwa inapambana kupanda juu ikilenga kumaliza katika nafasi ya tatu bora.

Licha ya kutokuwepo kwa nahodha wao John Terry,  ambaye anauguza jeraha la goti, mshambulizi Fernando Torres ambaye amekuwa akiifungia Chelsea mabao katika mechi kadhaa zilizopita anatarajiwa kuendeleza rekodi hiyo.

Kocha wa Manchester City, Roberto Mancini huenda akamchezesha Carlos Tevez kwa mara ya kwanza tangu mwezi Septemba mwaka uliopita baada ya kumpiga marufuku kwa sababu za kinidhamu.

Katika mechi zingine Jumatano usiku, Tottenham watakuwa wenyeji wa Stoke City,Everton watakuwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Goodison Park dhidi ya Arsenal,wakati Queens Park Rangers wakichuana na Liverpol.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.