Pata taarifa kuu
Uingereza

Roberto Mancini aonesha matumaini ya kunyakua Kombe la michuano ya ligi kuu Uingereza

Kocha wa Manchester City, Roberto Mancini ana matumaini makubwa kuwa watakuwa mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza, lakini amesema kuwa mechi tatu walizozibakiza zitathibitisha nafasi yao katika ligi hiyo.

Kikosi cha Manchester City
Kikosi cha Manchester City Reuters
Matangazo ya kibiashara

Manchester City ilipoteza mchezo baada ya kufungwa bao 1 kwa 0 na Swansea siku ya jumapili, huku Manchester United ikiwa juu yao baada ya ushindi wa mabao 2 kwa 0 dhidi ya West Bromwich Albion.

Ingawa Mancini amekiri kuwa na wakati mgumu,amesema hiyo ndio namna mashindano ya Mpira yalivyo lakini ameonesha kuwa ana uhakika wa kupata taji la kwanza ndani ya miaka 44.

Mancini amesema ingawa wako nyuma ya Manchester United, lengo lao la ushindi halijabadilika wakati huu wakiwa wamebakiza michezo 10.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.