Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Kocha Rafa Benitez apewa nafasi kubwa ya kukinoa kikosi cha Chelsea

Ikiwa zimepita siku mbili toka klabu ya Chelsea imfukuze kocha wake mkuu Andre Villa Boas kufuatia kipigo cha bao moja kwa nunge mwishoni mwa juma toka kwa klabu ya Westbrownch Albion, klabu hiyo imeanza mchakato wa kumsaka mrithi wa kiti hicho.

Kocha Rafa Benitez anayepewa nafasi kubwa ya kuifundisha klabu ya Chelsea
Kocha Rafa Benitez anayepewa nafasi kubwa ya kuifundisha klabu ya Chelsea Reuters
Matangazo ya kibiashara

Makocha kadhaa wameanza kutajwa kuweza kuchukua nafasi ya kukinoa kikosi hicho aiwemo kocha wa zamani wa klabu hiyo Josee Mourinho, Pep Guardiola ambaye ni kocha wa FC Barcelona pamoja na Rafael Benitez aliyewahi kukinoa kikosi cha Liverpool.

Kufuatia mchakato huo kocha wa zamani wa Liverpool Rafa Benitez ameweka wazi msimamo wake wa kutaka kufundisha moja ya vilabu ambavyo vinania ya kuendelea kutwaa vikombe ikiwemo klabu ya Chelsea licha ya kushindwa kuthibitisha kama anataka kujiunga na klabu hiyo.

Benitez amesema kuwa malengo ya kocha yoyote bora ni lazima kuhakikisha kuwa anapata klabu bora ya kuifundisha ili kuweza kuleta furaha kwa mashabiki wa klabu husika.

Kocha huyo ambaye amekuwa hana timu kwa muda mrefu sasa amesema kuwa endapo atapata timu yenye msimamo mzuri na iko kwenye nafasi ya kuweza kutwaa mataj basi atakuwa hana hiyana kuweza kuichukua klabu hiyo.

Kwa upande wake kocha wa Real Madrid Josee Mourinho amesema kuwa kwasasa hawezi zungumza chochote kuhusu kuhamia klabu hiyo na kusisitiza kuwa ni nani ambaye hapendi kufundisha klabu bora kama Real Madrid japo uamuzi ni wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.