Pata taarifa kuu
Chelsea-NAPOLI

Kitim tim leo baina ya Chelsea na Napoli

Leo patawaka moto katika dimba la San Paolo wakati ambapo Chelsea wataumana na Napoli, mchezo huu unataraji kuwa mzuri kutokana na kwamba mashabiki wa soka wanaeleza kuwa kurejea kwa Napoli katika klabu bingwa Ulaya tena katika hatua ya mbele zaidi, kunamaanisha vitu vingi sana kwa mashabiki wa mji huo ambao wanaishi kwa ajili ya soka

kocha wa Chelsea Andre Villas-Boas na Didier Drogba l
kocha wa Chelsea Andre Villas-Boas na Didier Drogba l REUTERS/Tony Gentile
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza siku moja kabla ya mchezo huo manager wa klabu ya Chelsea Andre Villas-Boas amesistiza kuwa anakitengeneza upya kikosi chake kwa ajili ya kudumisha mafanikio waliyonayo.

Andre Villas Boas amesikika akijigamba nakusema kwamba Stamford bridge ni uwanja mzuri na ndio maana wanataka kuongoza katika kundi lao na kuelekea katika nafasi hiyo watahakikisha wanafanya kile walichokifanya katika dimba la stamford bridge ili kuhakikisha wanaendeleza ushindi.

Wakati huo huo timu ya Chelsea imearifiwa kuhusu tuhuma za kibaguzi kutoka kwa baadhi ya wanatimu, ambapo msemaji wa timu hiyo alisema kuwa kama itabainika kuwa mmoja waoa anahusika na tuhuma hizo basi timu nzima italiona hilo kama jambo lisilo kubalika.

 

 

hayo yakiripotiwa

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.