Pata taarifa kuu
ZAMBIA

Timu ya Taifa ya Zambia yalakiwa kishujaa baada kutwaa ubingwa Afrika

Timu ya Taifa ya soka ya Zambia ambayo ndiyo bingwa mpya imelakiwa kishujaa baada ya kurejea nyumbani ikiwa na Kombe la Mataifa ya Afrika ililolitwaa katika fainali iliyopigwa nchini Gabon juzi.

© Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mashabiki waliokuwa wakisubiri timu hiyo maarufu kama Chipolopolo, walijawa na furaha na uwanja wa ndege mjini Lusaka uligubikwa na nderemo kutoka kwa mashabiki hao.

Nderemo hiozo zilinoga hasa baada nahodha Christopher Katongo alipoteremka kutoka ndani ya ndege akiwa amebeba Kombe hilo.

Timu ya Taifa ya soka ya Zambia, 'Chipolopolo' juzi ilifanikiwa kuandika historia katika soka barani Afrika baada ya kuifumua Timu ya Taifa ya Cote D' Ivoire kupitia mikwaju ya penati nane kwa saba8-7 katika mchezo wa fainali uliofanyika nchini Gabon.

Timu hizo zililazimika kupigiana mikwaju ya penati baada ya kutoka bila kufungana katika dakika 90 za kawaida na baadaye dakika 30 za ziada mambo yakawa vilevile.

Hata hivyo katika kipindi cha kawaida Cote D' Ivoire ilibidi wajilaumu wao baada ya nahodha wao Didier Drogba kukosa penati katika kipindi cha kwanza na kuwaacha mashabiki wa timu yake wasiamini kile kilichotokea.

Katika vipindi vyote timu zote zilikua zikishambuliana vikali lakini nyavu hazikuweza kutikiswa huku magolikipa wote wakionyesha umahiri wao katika kunyakua mipira iliyokuwa ikielekezwa langoni mara kwa mara.

Penati ya mwisho ya mchezaji Stoppila Sunzu wa Zambia ndiyo iliandika historia hiyo baada ya mchezaji huyo kupiga na kupata kufuatia mchezaji wa Zambia na mshambuliaji wa Arsenal Gervinho kukosa penati iliyotangulia.

Mchezo huo kwa Zambia ulikuwa na lengo la kuweka kumbukumbu kwa ajili ya wachezaji 18 wa timu hiyo walifariki kwa ajali ya ndege nchini Gabon.

Ushindi huo kwa Zambia umekuwa wa kihistoria baada ya wachezaji wa timu hiyo kunuia kupata ubingwa huo kwa ajili ya kuwaenzi wachezaji hao wa zamani wa Zambia waliofariki katika ajali hiyo ya ndege.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.