Pata taarifa kuu
Gabon

Wachezaji wa Zambia wawasili Nchini Gabon tayari kumenyana na Cote d' Ivoire siku ya Jumapili

Timu ya taifa ya Zambia imewasili nchini Gabon Tayari kwa mchezo wa kukata na mundu katika fainali dhidi ya Cote de Voire siku ya Jumapili. 

Wachezaji wa Zambia wakitoa heshima zao kwa wachezaji waliopata aj
Wachezaji wa Zambia wakitoa heshima zao kwa wachezaji waliopata aj REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kuwasili nchini Gabon, timu hiyo imekwenda katika ufukwe wa bahari ya Atlantic mjini Libriville na kutoa heshima zao kuwakumbuka wachezaji wa timu ya taifa waliopoteza maisha katika ajali ya ndege tarehe 27 mwezi Aprili mwaka 1993.

ajali hiyo ilitokea wakati wakienda kushiriki michuano ya kufuzu kushiriki Kombe la dunia nchini Senegal ambapo walitua nchini Gabon kuweka mafuta na muda mfupi baada ya ndege kuruka ndege hiyo ilianguka majini na kusababisha vifo vya watu wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

Nahodha wa timu hiyo Kalusha Bwalya ndiye aliyesalimika katika ajali hiyo na Anasema miaka hiyo ya tisini ni kama jana tu kutokana na timu hiyo na jinsi ambavyo walifanya kazi kwa pamoja na kila mtu alifanya bidii katika timu hiyo kwa ajili ya timu ,pia anahisi furaha kwamba waliweza kuunganisha timu mpya na ile ya ya zamani na anaamini vijana wanafahamu kiapo cha wachezaji waliopoteza maisha katika pwani hiyo ya Gabon.

Kocha wa timu ya taifa ya Zambia, Goran Stevanovic Anasema kwamba uwezekano wa wao kurejea nchini Gabon ilikuwa ni kucheza na kutinga katika fainali jambo ambalo wamefanikisha hivyo kilichobaki ni wao kutwaa kombe kwa ajili ya kuwaenzi wote waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo.

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.