Pata taarifa kuu
Uingereza

Michuano ya Ligi kuu ya Uingereza kuwakutanisha Tottenham na Newcastle

Kocha wa Tottenham Hotspur Harry Redknapp anatarajiwa kukaribishwa vyema wakati huu anapoiongoza timu yake katika Mechi yake ya nyumbani dhidi ya Newcastle, mtanange utakaopigwa Kesho.

Kocha wa Timu ya Tottenham Hotspur, Harry Redknapp
Kocha wa Timu ya Tottenham Hotspur, Harry Redknapp REUTERS/Luke MacGregor
Matangazo ya kibiashara

Saa chache siku ya Jumatano, Redknapp alithibitishwa kuwa hakua na hatia baada ya kuingia kwenye shutma za kukwepa kulipa kodi, ambapo iwapo angethibitishwa kuwa na makosa angefifisha matumaini yake ya kuwa Kocha wa Timu ya Taifa ya Uingereza, wakati huu ambapo anatazamiwa kuwa pengine atairithi nafasi ya Fabio Capello baada ya Muitaliano huyo kujiuzulu.
 

Lakini wakati kukiwa na shuku juu ya Redknapp kuongoza Timu ya Taifa ya Uingereza katika Michuano ya Yuro mwaka 2012 nchini Ukraine na Poland.
 

Fabio Capello alijiuzulu kuoinga uamuzi wa FA kumvua unahodha wa timu ya Taifa ya nchi hiyo John Terry kwa shutma za kuhusika na vitendo vya kibaguzi shutma ambazo Terry amezipinga.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.