Pata taarifa kuu
Gabon

Mali na Ghana zafuzu hatua ya nusu fainali katika mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika

Mali na Ghana zimefanikiwa kuingia kwenye Nusu fainali baada ya kuzishinda Gabon na Tunisia katika mashindano ya mpira wa miguu ya Kombe la Mataifa ya Afrika, uliopigwa jana.

John Mensah wa Ghana akipambana na Sabeur Khalifa wa Tunisia katika mpambano wa jumapili
John Mensah wa Ghana akipambana na Sabeur Khalifa wa Tunisia katika mpambano wa jumapili
Matangazo ya kibiashara

Mali ilitinga nusu fainali kwa mtindo wa matuta kwa kupata magoli 5 dhidi ya 4 ya Gabon, katika mchezo wa robo fainali.
 

Ghana ilipata ushindi mwembamba na kuepuka msuko suko wa mikwaju ya Penati kwa kuishinda Tunisia kwa Magoli 2 kwa 1 katika muda wa nyongeza, katika mchaezo uliomalizika huku ukitawaliwa na ghadhabu na Timu ya Tunisia wakisalia wachezaji 10.

Kocha msaidizi wa timu ya Ghana, Kwesi Appiah ameonesha furaha yake ya kuingia katika awamu ya nusu fainali lakini amekemea vitendo vya wachezaji wa Timu ya Tunisia kwa kuugeuza mchezo baina yao kuwa vita na kutaka mamlaka kuchukua hatua kukomesha vitendo vya vurugu uwanjani, vitendo vinavyoleta ishara mbaya kwa mashindano ya Mpira wa Miguu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.