Pata taarifa kuu
ZAMBIA

Zambia yapania kutinga nusu fainali

Timu ya Zambia imepania kutinga hatua ya nusu fainali katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika ambapo watakuwa na kibarua cha aina yake kitakachowakutanisha na timu ya Sudan katika dimba la Estadio de Bata jumamosi jioni.

Kikosi cha Zambia wana Chipolopolo
Kikosi cha Zambia wana Chipolopolo RFI/Issouf Sanogo
Matangazo ya kibiashara

Katika kumbukumbu za wana Chipolopolo hao walitolewa nje mnamo mwaka 2010 katika hatua ya robo fainali huko Angola na sasa wamejipanga kupiga hatua zaidi.

Vijana hao wanaopata mafunzo chini ya usimamizi wa kocha Herve Renard' walifanikiwa kuongoza kundi A wakiwaacha mbali Guinea ya Ikweta,Libya na Senegal pasipo kufungwa huku wakiwa na ushindi mara mbili na sare.

Hata hivyo Zambia ina kibarua kigumu cha kuikabili timu ya Sudan ambayo kwa upande wake imejiweka katika nafasi nzuri ya kufanya vizuri nayo ikiwa imeshathubutu mara kadhaa kufikia hatua ya mtoano.

Msakata kabumbu Rainford Kalaba amekuwa akifanya vizuri kwa Zambia wakati nahodha Christopher Katongo amekuwa mfano na wachezaji wote wawili watakuwa wakisaka kuendeleza mashambulizi dhidi ya timu hatari ya Sudani.

Zambia itakipiga pasipo mchezaji wake Clifford Mulenga ambaye amerejeshwa nyumbani kwa sababu za utovu wa nidhamu jambo ambalo hata hivyo halitayumbisha mpambano huo.

Kwa upande wa Sudan,kijana Mohamed Bashir aliwahi kuwa shujaa aliyeipatia timu hiyo ushindi wa sare kwa bao 2-2 walipochapana na timu ya Angola.

Kocha wa Zambia Herve Renard amesema kuwa anatarajia mchezo uliojaa changamoto sana kutoka kwa vijana hao wa Sudan lakini ana imani kila kitu kitakwenda vizuri hata kama Sudan haitawapa nafasi ya kupoteza kwa kuwa ni mpambano wa kutinga nusu fainali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.