Pata taarifa kuu
UINGEREZA

John Terry avuliwa unahodha wa timu ya taifa ya Uingereza

Chama cha soka nchini Uingereza FA kimetangaza kumvua rasmi unahodha wa timu ya taifa ya Uingereza beki wa kati wa timu ya Chelsea na timu ya taifa ya nchi hiyo John Terry kufuatia mchezaji huyo kuandamwa na kashfa ya ubaguzi wa rangi.

Nahodha wa timu ya Taifa ya Uingereza, John Terry akiwa kwenye moja ya mazoezi ya timu yake
Nahodha wa timu ya Taifa ya Uingereza, John Terry akiwa kwenye moja ya mazoezi ya timu yake Reuters
Matangazo ya kibiashara

Taarifa za kuvuliwa rasmi unahodha wa timu ya Tiafa ya Uingereza zimethibitishwa na mkurugenzi wa chama cha soka nchini humo FA, David Bernstein ambaye amesema kuwa wameamua kufikia uamuzi huo baada ya kuona kuna umuhimu wa kufanya hivyo.

Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa kutokana na kesi ambayo iko mbeleni ikimkabili mchezaji huyo na wao kuwa na michuano mikubwa ya kombe la ulaya hapo mwakani, wanadhani ni wakati mufaka wakumvua unahodha mchezaji huyo ili kupisha kesi inayomkabili kuendelea.

Hivi karibuni polisi nchini humo walisema kuwa wamekamilisha kukusanya ushahidi ambao unamuhusisha nahodha huyo wa Chelsea na tukio la kutoa maneno ya kibaguzi dhidi ya beki wa QPR Antonio Ferdinand wakati timu hizo zilipokutana kwenye mchezo wa ligi kuu.

Terry ambaye awali walivuliwa unahodha baada ya kupatikana na hatia ya kutembea na mke wa mchezaji mwenzake alirejeshewa cheo hicho baada ya kuonekana licha ya kufanya kosa hilo lakini alistahili kubakia kuwa nahodha.

Kwa mujibu wa taarifa ya chama hicho imesema kuwa mchezaji huyo hatokuwa nahodha wa timu hiyo mpaka pale kesi ambazo zinamkabili zitakapomalizika.

John Terry mwenyewe ameendelea kukanusha kuhusu tuhuma zinazomkabili na kusema kuwa hana hatia ya tukio lolote na atathibitisha hilo mahakamani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.