Pata taarifa kuu
LIGI KUU YA UINGEREZA

Arsenal yaendelea kuvutwa shati katika ligi kuu ya Uingereza

Ligi kuu ya nchini Uingereza imeendelea kushika kasi wakati huu ambapo imeingia katika mzunguko wake wa pili huku baadhi ya timu zikianza kuonyesha nia kutaka kutwaa ubingwa wa ligi hiyo pamoja na kusalia kwenye ligi kuu msimu ujao.

Mchezaji wa Arsenal Robin Van Persie akijaribu kufunga goli dhidi ya Bolton, timu hizo zilitoka sare ya 0-0
Mchezaji wa Arsenal Robin Van Persie akijaribu kufunga goli dhidi ya Bolton, timu hizo zilitoka sare ya 0-0 Reuters
Matangazo ya kibiashara

Katika mechi ambazo zilichezwa hapo jana, timu ya Aston Villa ilikuwa wenyeji wa QPR katika mchezo ambao umeshuhudia timu hizo zikitoka sare ya mabo 2-2 huku klabu ya Fulham nayo ikilazimishwa sare ya bao 1-1 na klabu ya West Bromwich.

Mechi nyingine za ligi hiyo ilizikutanisha timu za Blackburn Rovers ambao walikuwa na kibarua dhidi ya Newcastle kwenye mchezo ambao umeshuhudia Newcastle wakipata ushindi wa mabao 2-0 na hivyo kuchumpa hadi kwenye nafasi tano kwenye msimamo wa ligi kuu.

Mchezo mwingine ambao ulikuwa unatazamwa na watu wengi ni ule uliozikutanisha timu ya Bolton ambayo walicheza na Arsenal na kushuhudia timu hizo zikishindwa kutambiana kwa kutoka sare ya bila kufungana na kuendelea kumuweka pabaya kocha mkuu wa Arsenal, Arsene Wenger ambaye anashinikizo kwa timu yake kupata ushindi.

Wakati Arsena wakiendelea kuvutwa shati timu ya Sunderland inayonolewa na kocha wake mpya Martin O'neil ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Norwich na kuendelea kusogea juu katika msimamo wa ligi hiyo.

Mpaka sasa msimamo wa ligi hiyo unaonesha Manchester City ikiendelea kuongoza wakiwa na alama 54 sawa na kalbu ya Manchester United yenye alama 54 ila wakitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.

Tottenham ni ya tatu wakiwa na alama 49 wakati Chelsea wakifuatia wakiwa na alama 42, Newcatsle United wao wako nafasi ya tano wakiwa na alama 39.
Timu ambazo zinashikiliwa mkia kwa sasa ni Wigan, Wolvehmapton na Blackburn.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.