Pata taarifa kuu
LIGI KUU YA UINGEREZA

Manchester City na Manchester United wakabana koo kileleni mwa ligi kuu ya Uingereza

Ligi kuu nchini Uingereza imeendela usiku wa kuamkia Jumatano na kushuhudia vinara wa ligi hiyo Manchester City wakipoteza mchezo wao dhidi ya Everton na kuwafanya walingane pointi na majirani zao Manchester Uinted.

Mchezaji Darron Gibson akiifungia bao timu yake ya Everton dhidi ya Man City
Mchezaji Darron Gibson akiifungia bao timu yake ya Everton dhidi ya Man City Reuters
Matangazo ya kibiashara

Everton ambao walikuwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Goodison Park waliwakaribisha vinara wa ligi hiyo klabu ya Manchester City kwenye mchezo ambao wengi walitarajia kuona Man city wakiibuka na ushindi lakini matokeo yakawa tofauti baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0.

Goli la Everton lilipatikana katika dakika ya 60 mchezo likifungwa na Darron Gibson alieytumia vema makosa ya mabeki wa Man City.

Mara baada ya mchezo huo kocha wa Man City, Roberto Mancin amesema kuwa hakuridhishwa na matokeo hayo wala jinsi wachezaji wake walivyocheza lakini hajakata tamaa ya kuendelea na mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu.

Mechi nyingine ilikuwa ni baina ya Manchester United waliokuwa katika uwanja wake wa nyumbani wa Old Traford kuwakaribisha timu ya Stoke City, na kushuhudia timu hiyo ikibanana kileleni na mahasimu wao Manchester City kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Magoli ya Man United yalifungwa na Javier Chicharito na lile la ushindi likifungwa na Mbulgaria Dimitry Berbatov na kumfanya kocha mkuu wa timu hiyo Sir Alex Fergason kuondoka na kicheko.

Mechi nyingine ni kuwa Tottehan wakawafungwa mabao 3-1 timu ya Wigan, wakati Chelsea wakilazimishwa sare ya bao 1-1 na timu ya Swansea huku Liverpool wakipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Wolveshampton.

Hii leo Arsenal watacheza na Bolton wakati Newcastle watakuwa wenyeji wa Blackburn Rovers.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.