Pata taarifa kuu
GABON-GINE YA IKWETA

Gabon yafuzu kwakishindo hatua ya robo fainali AFCON 2012

Michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika imeendelea kushika kasi kwa timu mbalimbali kufanikiwa kufuzu kucheza hatua ya robo fainali huku ikishuhudiwa vigogo wakishindwa kutamba.

Pierre Aubameyang mchezaji wa Gabon akishangilia bao la ushindi aliloifungia timu yake
Pierre Aubameyang mchezaji wa Gabon akishangilia bao la ushindi aliloifungia timu yake CAF Online
Matangazo ya kibiashara

Katika mechi za hapo jana, timu ya taifa ya Niger ilikuwa na kibarua dhidi ya timu ya taifa ya Morocco katika mchezo ambao umeshuhudia timu ya taifa ya Morocco licha ya kupata ushindi wa bao 1-0 haikufanikiwa kusonga mbele.

Bao pekee la Morocco lilifungwa katika dakika ya 79 ya mchezo na mchezaji Younes Belhanda na hivyo kupata ushindi wake wa kwanza kwenye mashindano ya mwaka huu.

mchezo mwingine uliwakutanisha wenyeji timu ya taifa ya Gabon ambao wao waliwakaribisha timu ya taifa ya Tunisia na kufanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0, bao likifungwa na mshambuliaji Pierre Emerick Aubameyang.

kwa matokeo ya hapo jana ya kundi C, timu ya taifa ya Gabon inangoza kundi lake ikiwa na alama 9 ikifuatiwa na timu ya taifa ya Tunisia yenye alama 6 na hivyo kuwa timu zilizofanikiwa kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya mwaka huu.

Mechi nyingine ambazo zitapigwa hii leo ni pamoja na Botswana watakaokuwa wenyeji wa Mali huku timu ya taifa ya Ghana watamaliza mechi yake kwa kucheza na timu ya taifa ya Guinea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.