Pata taarifa kuu
AUSTRALIA

Murray na Djokovic kukabiliana kwenye Nusu Fainali ya Australian Open

Mchezaji Tennis nambari nne kwa ubora duniani Andy Murray amefanikiwa kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Mashindano ya Australian Open baada ya kumfunga Kei Nishikori na anatarajiwa kupambana na Novak Djokovic.

REUTERS/Toby Melville
Matangazo ya kibiashara

Murray raia wa Uingereza amefanikiwa kushinda mchezo wake wa Robo Fainali kwa kumshinda Nishikori kwa seti tatu kwa bila na kufanikiwa kutinga hatua ya Nusu Fainali ya mashindano ya Australian Open kwa mara ya tatu mfululizo.

Murray ameshinda kwa matokeo ya 6-3 6-3 6-1 na hivyo kukata tiketi ya kupambana na Djokovic kirahisi tofauti na ambavyo wenhi walidhani angekabiliana na upinzani mkali kutoka kwa mpinzani wake Nishikori.

Baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Mashindano ya Australian Open Murray amesema japokuwa hakucheza kwenye kiwango ambacho alikuwa anakitaka lakini matokeo yamekuwa mazuri kwake.

Naye Mchezaji nambari moja kwa ubora wa tennis upande wa wanaume Novak Djokovic amefanikiwa kumsambaratisha David Ferrer na kutinga Nusu Fainali na sasa atakabiliana na Murray.

Bingwa Mtetezi wa Taji la Australian Open Djokovic amefanikiwa kumsambaratisha Ferrer kwa seti tatu bila ya jibu na kuweza kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kuweza kutetea ubingwa wake.

Djokovic amefanikiwa kupata matokeo ya 6-4 7-6 6-1 na baada ya mchezo huo amesema atajitahidi kucheza kama ilivyokuwa mwaka jana dhidi ya Murray ili aweze kutinga fainali kwa mara nyingine.

Nusu Fainali nyingine inatarajiwa kuwakutanisha Roger Federer na Rafael Nadal mchezo mwingine wa kisasi ambao utaamua nani mbabe kati ya wawili hao ambao wanawania ubingwa wa mwaka huu kwa udi na uvumba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.