Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Klabu ya Liverpool yaeleza kutoridhishwa na adhabu aliyopewa mchezaji wake Luis Suarez

Chama cha soka nchini Uingereza FA hatimaye kimetoa adhabu kali kwa mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Luis Suarez baada ya kumkuta na hati ya kutoa matamshi ya kibaguzi dhidi ya mchezaji wa Manchester United Patrice Evra.

Luis Suarez (kulia) na Patrice Evra (kushoto)
Luis Suarez (kulia) na Patrice Evra (kushoto) REUTERS/Phil Nobl
Matangazo ya kibiashara

FA imemkuta na hatia mchezaji huyo baada ya kuridhika na ushahidi wa picha za video ambazo zilimuonesha mshambuliaji huyo akitamka maneno ya kibaguzi dhidi ya mchezaji wa Manchester United Patrice Evra.

Katika hukumu hiyo FA imemfungia mchezaji huyo kucheza mechi nane pamoja na kumtaka kulipa faini ya paundi elfu arobaini na kumpa muda wa siku kumi na nne kukata rufaa endapo ataona haridhiki na maamuzi yaliyofikiwa.

Mara baada ya kutolewa kwa adhabu hiyo, pia chama cha wachezaji wa kulipwa nchini humo kimepingeza uamuzi wa FA kikisema kuwa kamwi vitendo vya kibaguzi haviruhusiwi mchezoni na kuwa haitakaa kimya kukemea vitendo hivyo.

Tayari klabu ya Liverpool imetoa taarifa kuonyesha kutoridhishwa na adhabu hiyo na kuahidi kukata rufaa.

Katika sakata la mchezaji wa klabu ya Chelsea ya Uingereza nahodha John Terry, hatimaye uchunguzi wa kesi yake umekamilika na waendesha mashtaka wameirdhishwa na ushahidi walionao na kwamba mchezaji huyo atapanda kizimbani mwezi wa pili mwakani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Terry anatuhumiwa kumtolea maneno machafu mchezaji wa QPR Anton Ferdinand wakati timu hizo zilipokutana mwezi wa kumi mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.