Pata taarifa kuu
LIGI KUU YA UINGEREZA

Manchester City yaendelea kukalia usukani wa Ligi kuu ya Uingereza

Klabu ya Manchester City ya nchini Uingereza hatimaye imefanikiwa kurejea kileleni mwa ligi hiyo baada ya nafasi hiyo kushikiliwa kwa muda na mahasimu wao manchester United.

David Silva akishanglia bao alilofunga, akipongezwa na Sergio Aguero
David Silva akishanglia bao alilofunga, akipongezwa na Sergio Aguero Reuters
Matangazo ya kibiashara

Manchester City walifanikiwa kurejea kileleni mwa ligi hiyo baada ya kufanikiwa kuwasambaratisha washika bunduki wa jiji la London klabu ya Arsenal kwa kuwacahapa bao moja kwa nunge.

Katika mchezo huo ambao ulivuta hisia za mashabiki wengi wa soka, hasa ukizungatia umuhimu wa mchezo huo kwa Manchester City na hata Arsenal yenyewe ulipigwa katika dimba la City of Manchester.

Bao peke na laushindi la Manchester City liliwekwa kimiani na mshambuliaji wake David Silva baada ya kutumia vema makosa ya mabeki wa arsenal walioshindwa kuokoa mpira uliotemwa na mlinda mlango wao kufuatia shuti kali la Mario Barloteli.

Awali usukani wa ligi hiyo ulikaliwa kwa muda na mashetani wekundu Klabu ya Manchester Uinted ambao walifanikiwa kuwasambaratisha QPR kwa mabao mawili kwa bila, magoli yakifungwa na Wyne Rooney pamoja na Michael Carrick.

Kwa matokeo hayo hivi sasa Manchester City itaendelea kuwa kileleni mwa ligi hiyo kwakujikusanyia alama 41 wakati Manchester United wenyewe wakiwa na alama 39, wakifuatiwa na klabu ya Tottenham Hotspurs yenye alama 34 huku wakifuatiwa na klabu ya Chelsea yenye alama 32.

Katika mechi nyingine Liverpool walifanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya Aston Villa, wakati Tottenham wakiwafunga Sunderland kwa bao moja kwa bila.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.