Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Chelsea yasitisha rekodi ya ushindi wa Manchester City kwenye Ligi Kuu Nchini Uingereza

Mkwaju wa penalty wa Kiungo wa Kimataifa wa Uingereza Frank Lampard ulitosha kuwapa ushindi Klabu ya Chelsea na kusitisha rekodi ya kipekee ambayo ilikuwa nayo Manchester City ya kutopoteza mchezo wowote kwenye Ligi Kuu Nchini Uingereza.

Matangazo ya kibiashara

Chelsea imefanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-1 mbele ya vinara wa Ligi Kuu Nchini Uingereza Manachester City ambayo ilikuwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo wowote hadi sasa kabla ya kukumbana na kisiki hicho usiku wa jumatatu.

Manchester City ndiyo walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia Mario Balotelli katika dakika ya pili ya mchezo kabla ya Chelsea haijasawazisha kupitia kiungo wake raia wa Ureno Raul Meireles akiunganisha kazi nzuri ambayo ilifanywa na Daniel Sturridge.

Chelsea wakiwa kwenye dimba lake la nyumbani la Stamford Bridge ilijikuta ikitawala mchezo kwa kiwango kikubwa baada ya Manachester City kumpoteza beki wake wa kushoto Gael Clinchy ambaye alilimwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya.

Katika dakika ya themanini na tatu ndiyo Chelsea walijipatia goli lao la tatu baada ya mwamuzi kuwazawadia penlaty baada ya Leon Lescott kuunawa mpira kwenye eneo la hatari baada ya Strurridge kupiga shuti lililoishia kwenye mkono wa mlinzi huyo.

Baada ya mchezo huo Kocha wa Chelsea ambaye alikuwa kwenye shinikizo kutokana na klabu yake kutokuwa na matokea mazuri Andre Villa-Boas amenukuliwa akisema kuwa timu yake bado ipo kwenye mbio za ubingwa baada ya kupata ushindi huo muhimu.

Villa-Boas amesema kwa sasa wanaendelea kuongeza kasi kwenye mbio za kusaka ubingwa lakini akakiri kama wangepoteza mchezo huo wangekuwa wamejiengua wenyewe kwenye kinyang'anyiro hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.