Pata taarifa kuu
MAREKANI

Novak Djokovic afanikiwa kusonga mbele kwenye mashindano ya US Open

Mchezaji nambari moja kwenye mchezo wa Tennis upande wa Wanaume Novak Djokovic amefanikiwa kusonga mbele kwenye Mashindano ya US Open kwa kumuondoa mpinzani wake Carlos Berlocq.

Matangazo ya kibiashara

Ushindi wa Djokovic dhidi ya Berlocq uliomchukua dakika 90 na kushinda seti 3-0 kwa matokeo ya 6-0, 6-0 na 6-2 yamemfanya aweze kutinga katika mzunguko wa tatu wa US Open inayozidi kushika kasi.

Djokovic ameendelea na rekodi yake bora katika mwaka 2011 ya kuweza kushinda michezo 59 na kupoteza miwili kitu kilichomfanya azidi kujijengea heshima kubwa kwenye mchezo wa Tennis kwa sasa.

Mpinzani wake raia wa Argentina, Berlocq baada ya kuchakazwa kwa seti 3-0 hakusita kumwagia sifa Djokovic na kusema kiwango ambacho kimeoneshwa na kijana hiyo kinadhihirisha anatoka nje ya dunia.

Berlocq ambaye anaorodheshwa katika nafasi ya 74 amesema kila mbinu ambazo alikuwa anatumia kukabiliana na Djokovic zilikuwa zinagonga mwamba na kudhihirisha mnchezji huyo ni mahiri.

Naye mchezaji nambari tatu kwa ubora duniani Roger Federer amefanikiwa kusonga mbele baada ya kumuondoa Dudi Sela mchezaji nambari 93 kwa kumfunga seti 3-0 kwa matokeo ya 6-3, 6-2 na 6-2.

Upande wa wanawake wanadada Serena Williams naye amefanikiwa kufuzu kwa hatua inayofuata baada ya kumuondoa kwenye mashindano Michaella Krajicek kwa seti 2-0 kwa matokeo ya 6-0 na 6-1.

Serena anatarajiwa kukabiliana na Victoria Azarenka ambaye alimshinda Gisela Dulko kwa seti 2-0 kwa kichapo cha 6-4 na 6-3.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.