Pata taarifa kuu
LIGI KUU YA UINGEREZA

Kitimtim cha ligi kuu ya Uingereza kuendelea wikiendi hii

Ligi kuu ya nchini Uingereza inatarajiwa kuendelea kutimua vumbi wikiendi hii kwa kushuhudia miamba mbalimbali ikishuka viwanjani huku tayari vijogoo vya jiji Liverpool wakikalia usukani wa Ligi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Katika mechi zilizochezwa siku ya jumamosi ya tarehe 27, imeshuhudiwa klabu ya Aston Villa ikilazimishwa sare ya bila kufungana na klabu ya Wolverhampton, huku Wigan wao wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Queens Park Rangers.

Mchezo mwingine uliwakutanisha timu ya Blackburn ambao walijikuta wakishindwa kutamba mbele ya Everton kwa kukubali kipigo cha bao 1-0, wakati matajairi wa London klabu ya Chelsea wakiibuka na ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya Norwich.

Katika mchezo huo ulishuhudia mchezaji Didier Drogba akikumbana na dhoruba baada ya kukongana na mlinda mlango wa Norwich, Ruddy na kusababisha kukimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi.

Swansea wao walilazimishwa sare ya 0-0 na klabu ya Sunderland, huku Liverpool wakichomoza na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Bolton na kukaa kileleni mwa ligi hiyo.

Hii leo kutakuwa na mechi kadhaa zitakazochezwa lakini ile ambayo imevuta hisia za watu wengi ni kati ya mashetani wekundu Manchester United watakaokuwa na kibarua dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Old Traford.

Tayari mashabiki wa pande zote mbili wameanza kutambiana kwa kila mmoja timu yake kuibuka na ushindi huku wengi wakiangalia historia ya timu hizo zinapokutana katika uwanja wa Old Traford ambako Arsenal imepoteza michezo mingi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.