Pata taarifa kuu
Michezo, Tennis

Serena Williams bingwa wa zamani wa taji la US Open atajwa kwenye nafasi ya 20

Bingwa mara tatu wa zamani wa Taji la US Open kwa upande wa wanawake Serena Williams ametajwa kwenye nafasi ya ishirini na nane wakati huu ambapo mashindano hayo yanatarajiwa kuanza juma lijalo.

Serena Williams akifumbatia taji lake
Serena Williams akifumbatia taji lake (Photo : Reuters)
Matangazo ya kibiashara

Hii ni mara ya kwanza kwa Serena kuorodheshwa kwenye nafasi ya chini namna hiyo licha ya hivi karibuni kufanikiwa kutwaa taji la Toronto na Stanford na akipambana kuhakikisha anarejea kwenye kiwango chake.

Nafasi ya kwanza imekwenda kwake Caroline Wozniacki wakati Vera Zvonareva akishika nafasi ya pili huku nafasi ya tatu ikiangukia kwake Maria Sharapova na tayari Bingwa Mtetezi Kim Clijsters amejiondoa kutokana na kukabiliwa na maumivu ya misuli ya tumbo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.