Pata taarifa kuu
Uingereza

Matokea mbalimbali ya ligi kuu ya Uingereza

Newcastle imetoka sare ya 0-0 na Arsenal katika mchezo uliokuwa na kasoro za hapa na pale. huku Liverpool ikitoka sare ya bao moja kwa moja na Sunderland, na QPR  ikatandika mabao 4 kwa sufuri na Bolton.

Wachezaji  Joey Barton et Gervinho wakishikana mashati wakati wa mechi baina ya Newcastle-Arsenal.
Wachezaji Joey Barton et Gervinho wakishikana mashati wakati wa mechi baina ya Newcastle-Arsenal. REUTERS/Nigel Roddis
Matangazo ya kibiashara

Katika mchezo Baina ya Arsenal na Newcastle  mshambuliaji wa Arsenal kutoka Ivory Coast Gervinho alioneshwa kadi nyekundu baada ya kushikana mashati na Joey Burton wa Newcastle. Awali Burton alikanyagwa kwa makusudi na Alex Song, ingawa mwamuzi hakuona tukio hilo.

Arsenal licha ya kujaribu kucheza mtindo wao wa 'kuteleza' walishindwa kuivunja ngome ya Newcastle. Wakicheza bila ya Cesc Fabregas na Samir Nasri, Arsenal walionekana kupata tabu kutengeneza nafasi.

Wakati huohuo  mchezaji Sebastian Larsson alifunga bao maridadi sana la kusawazisha na kufanikiwa kuipatia timu yake ya Sunderland pointi moja dhidi ya Liverpool katika mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Soka ya England.

Liverpool ilikuwa ijipatie bao mapema, lakini mchezaji Luis Suarez alipiga mkwaju wa penalti ukapaa juu ya lango la Sunderland.

Sunderland katika kipindi cha kwanza hawakuonekana tishio sana langoni mwa Liverpool, lakini katika dakika ya 57 Larson alipata nafasi ya kuunganisha mkwaju wa pembeni uliopigwa na Ahmed El Mohammedy na kuisawazishia timu yake kwa bao safi sana huku ngome ya Liverpool ikiwa inamuangalia tu bila kumkabili.

Matokeo hayo yamezifanya timu hizo zigawane pointi moja.
 

Nayo QPR imeanza Ligi Kuu ya soka ya England kwa kupachikwa mabao manne huku Bolton ikiwafundisha soka katika mechi yao ya kwanza ya kufungua msimu wa Ligi Kuu ya England.

imu hiyo ya QPR ikicheza katika uwanja wa nyumbani ilicheza vizuri kipindi cha kwanza, lakini wakawa wanazorota kila muda ulivyokuwa ukiyoyoma.

Mabao hayo manne ya Bolton yalifungwa na Gary Cahill kwa mkwaju wa mbali kipindi cha kwanza, Danny Gabbidon mlinzi wa QPR akajifunga mwenyewe bao la pili na Ivan Klasnic akapachika bao la tatu.

Fabrice Muamba alikamilisha kitabu cha mabao kwa kufunga bao la nne, kabla ya mchezaji wa QPR kutolewa nje kwa kadi nyekundu.

Matokeo hayo yanaifanya Bolton kuanza ligi kwa kuongoza ikiwa na pointi 3 na mabao manne.

Wolverhampton Wanderers ikiwa ugenini imeshalazwa bao 1-0, ilijipapatua na kuweza kurejesha bao na hatimaye kufanikiwa kuilaza Blacburn mabao 2-1.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.