Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Klabu ya Chelsea yamtangaza Andre Villas-Boas kuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo

Hatimaye uongozi wa klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza umemtangaza rasmi aliyekuwa kocha wa FC Porto ya Ureno Andre Villas-Boas kuwa kocha mkuu mpya wa matajiri hao wa London.

Kocha mpya wa Chelsea, Andre Villas Boas
Kocha mpya wa Chelsea, Andre Villas Boas REUTERS/Grigory Dukor
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hiyo imetolewa hii leo na uongozi wa klabu ya Chelsea ikisema kuwa hatimaye wamafikiana na klabu ya Porto kuhusu uhamisho wa kocha huyo ambaye aliipa ubingwa wa ulaya timu hiyo.

Klabu ya Chelsea ililazimika kufunja mkataba wa kocha huyo na klabu ya Porto kwa kukubali kulipa paundi za uingereza milioni 13 kama fidia kwa klabu ya Porto kwa kuvunja mkataba na kocha wao.

Mapema juma hili ilibainika kuwa kocha huyo mara baada ya kupewa likizo na klabu yake alitumia muda mwingi nchini Uingereza ambako inaelezwa alikutana na viongozi wa Chelsea na kufanaya nao mazungumzo ya awali ambayo sasa yamezaa matunda.

Siku aya Jumanne, kocha Andre Villas-Boas alitangaza kubwaga manyanga kuifundisha klabu ya FC Porto hatua ambayo ilipokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa soka wa Porto akiwemo rais wa klabu hiyo ambaye aliweka wazi kuwa timu yake ilikuwa bado inamuhitaji kocha huyo kijana.

Andre Villas-Boas ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 33, amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuifundisha klabu hiyo yenye maskani yake mjini London na kuwa moja wa makocha vijana zaidi waliowahi kufundisha soka nchini Uingereza.

Wachambuzi wa Mpira wamesema kuwa huenda kocha huyo akakabiliwa na kibarua kigumu cha kuijenga timu hiyo iliyojaa wachezaji mahiri duniani ambao wengi wanaonekana kuwa umri sawa na kocha huyo akiwemo Frank Lampard na Didier Drogba.

wachambuzi hao wamesema kuwa kocha huyo ana kazi kubwa ya kufanya ambayo ilikuwa imeachwa na mtangulizi wake Carlo Anchelot aliyetimuliwa na klabu hiyo kwa kushindwa kuipa mataji.

Kocha huyo anatarajiwa kuanza kukinoa kikosi hicho muda wowote kuanzia sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.