Pata taarifa kuu
Ufaransa

Andy Murray, Rafael Nadal nusu fainali ya French Open.

Bingwa mtetezi wa mashindano ya mchezo wa Tennis ya French Open kwa upande wa wanaume, Rafael Nadal anacheza na Andy Murray kutoka Uingereza katika nusu fainali ya mashindano hayo yanayoendelea jijini Paris.Murray mwenye umri wa miaka 24 amesema ana mataumaini makubwa ya kushinda mchuano huu na kutinga katika awamu ya nusu fainali kwa mara ya kwanza wakati Nadal naye akisema ana matumaini anatarajia kupata ubingwa huo mara sita.

Uwanja wa Tennis
Uwanja wa Tennis Reuters
Matangazo ya kibiashara

Katika nusu fainali ya pili,Mswizi Roger Federer anapambana na Mserbia Novak Djokovic.
Fainali ya wanaume inachezwa Jumamosi hii kati ya bingwa mtetezi Francesca Schiavone kutoka Italia na Li Na kutoka China.
Schiavone alimshinda,Mfaransa Marione Bartoli mbele ya mashabiki wa nyumbani kwa seti 6-3 na 6-3 na kutinga katika fainali hiyo,huku Li Na,akimgaragaza Maria Sharapova kutoka Urusi kwa seti 4-4,7-5.
Fainali hiyo inatarajiwa kuwa ngumu kwa mujibu wa wachambuzi wa mchezo wa Tennis kutokana na uzoefu wa wachezaji hawa wawili.
Ikiwa Li Na atashinda mchuano huo atakuwa mchezaji wa kwanza kufanya vyema katika mashindano hayo katika siku za hivi karibuni,na ikiwa Schiavone anayenyakua ubingwa,atakuwa bingwa kwa mara mbili mfululizo.
Imeandaliwa na kocha mstaafu Victor Abuso.

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.