Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Liverpool yaishushia kipigo kizito Klabu ya Fulham

Magoli matatu yaliyofungwa na Kiungo wa Kimataifa wa Argentina Maxi Rodriguez na mengine mawili ya Dirk Kuyt na Luis Suarez yametosha kuwapa ushindi mnono wa magoli 5-2 Liverpool ambao walipambana na Fulham.

Golikipa wa Liverpool Pepe Reina akishangilia moja ya magoli ambayo timu yake imeshinda
Golikipa wa Liverpool Pepe Reina akishangilia moja ya magoli ambayo timu yake imeshinda
Matangazo ya kibiashara

Ushindi huu umeifanya Liverpool maarufu kama Vijogoo vya Jiji kushika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza na kukaribia kukata tiketi ya kushirikia michuano ya Europa Ligi.

Liverpool ambayo kwa sasa imekuwa mwiba hatari imefanikiwa kufunga magoli 13 katika michezo yake mitatu ya Ligi na hivyo kufanikiwa kujinasua toka nafasi ya 12 hadi nafasi ya 5.

Kiungo Rodriguez amefanikiwa kufunga magoli matatu kwa mara ya pili katika michezo mitatu aliyoshuka dimbani kuisadia timu yake kuvuna ushindi kwenye mchezo huo.
Katika mcheso hio ambao ulitawaliwa vilivyo na Liverpool imeshuhudia Fulham wakipata magoli yao kupitia Moussa Dembele na Steve Sidwell lakini hata hivyo hayakutosha kuwafanya waibuke wababe.

Licha ya kushika nafasi hiyo ya tano kwa sasa Liverpool bado hawana uhakika wa kushika nafasi hiyo kwa kuwa wapinzani wao wanaowania nafasi hiyo Tottenham Hotspur wanamchezo mmoja huku tofauti ya pointi ikiwa ni mbili.

Kocha wa Liverpool Kenny Dalglisha ambaye alichukua jukumu la kuinoa timu hiyo kutoka kwa mtangulizi wake Roy Hodgson amesema ameridhishwa na namna wachezaji wake wanavyojituma na kuwa chachu ya kuvuna ushindi.

Kwa upande wake Kocha wa Fulham Mark Hughes amekiri makosa ambayo wamefanya ndiyo ambayo yamekuwa sababu ya wapo kupata kichapo kizito kwenye mchezo huo.

Kwa sasa Ligi Kuu nchini Uingereza inaelekea ukingoni huku timu karibu zote zikiwa zimesalia na michezo miwili kasoro Tottenham Hotspur na Manchester City wenye michezo mitatu kila mmoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.