Pata taarifa kuu

Israel inajiandaa kwa jibu la 'nguvu na la maamuzi' baada ya shambulio la Iran

Iran imezindua Operesheni "Honest Promise", shambulio kubwa la ndege zisizo na rubani na makombora" dhidi ya Israeli ambalo limesababisha Waisraeli wengi kukimbilia kwenye maeneo salama jana usiku.

Video hii iliyorekodiwa na AFPTV mnamo Aprili 14, 2024 inaonyesha milipuko angani huko Hebroni, katika Maeneo ya Palestina, wakati wa shambulio la Iran dhidi ya Israeli.
Video hii iliyorekodiwa na AFPTV mnamo Aprili 14, 2024 inaonyesha milipuko angani huko Hebroni, katika Maeneo ya Palestina, wakati wa shambulio la Iran dhidi ya Israeli. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Jerusalem, Michel Paul

"Shambulio la Iran halijaisha" , kulingana na vyanzo kadhaa kutoka Israel leo Jumapili asubuhi. "Hata kama bado kuna kubwa zaidi nyuma yetu," anaongeza afisa wa kijeshi wa Israeli. Ni kwa mara ya kwanza, Iran kushambulia Israeli moja kwa moja, hata kama sehemu ya makombora yaliyorushwa kwa dola ya Kiyahudi yalitoka kwa washirika wa Iran, haswa Yemen, Iraq, Syria na Lebanon.

Ilikuwa ni shambulio kubwa: makombora 110 ya balestiki, makombora 36 ya cruise na ndege zisizo na rubani 185. Mamia ya makombora na ndege zisizo na rubani zimenaswa na Israel, Marekani, Jordan na Uingereza. Kulingana na Israeli, 99% ya vifaa ambavyo vilikuwa hatari vimeangamizwa. Vifaa vingi vilidondoka nje ya anga ya Israel. Kusini mwa Israeli na kambi ya kijeshi vimeshambuliwa. Na pia maeneo ya vijijini. Msichana mdogo amejeruhiwa kiasi. Na upande wa kaskazini, kwenye milima ya Golan, kambi nyingine ya jeshi imelengwa. Kombora lilipiga nyumba katika mji wa Katsrin, na kusababisha uharibifu mkubwa. Na kwa mujibu wa msemaji wa jeshi, shambulio la Iran bado halijaisha.

"Tutawapiga wale waliotupiga"

Swali sasa bila shaka ni jinsi Israeli itachukua hatua. Israel inasema inajiandaa kwa majibu ambayo inaahidi yatakuwa yenye nguvu na yenye maamuzi. Serikali imetoa idhni kwa makao makuu ya jeshi kuandaa majibu. Na baraza la mawaziri limepangwa kukutana tena baadaye leo.

"Tutawapiga wale waliotupiga," anasema Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu. "Tutaitikia kwa dhamira huku tukiwa tumetulia," ameongeza asubuhi ya leo.

Waziri Mkuu wa Israel alizungumza kwa simu kwa dakika 25 na rais wa Marekani. Inasemekana kuwa Israel imejitolea kuratibu majibu yoyote na Marekani, bila haraka. Lakini asubuhi ya leo, pia inadaiwa kuwa Joe Biden alisema anapinga shambulio lolote la Israel dhidi ya Iran. Netanyahu anatarajia kukutana na viongozi wengine. Nchini Israeli, wengi wanabaini kwamba mapambano dhidi ya Iran bado yako mbele kwa siku kadhaa.

Mwandishi wa wahariri anabainisha kuwa hii pia ni mara ya kwanza tangu vita vya kwanza vya Ghuba kwa Israel kushambuliwa na taifa huru. Wakati huo, mwaka wa 1991, ilikuwa Iraq. Na baadae, Israeli haikujibu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.