Pata taarifa kuu

Uturuki: Upinzani wapata mafanikio katika uchaguzi wa serikali za mitaa

Nairobi – Chama kikuu cha upinzani nchini Uturuki, kimeendelea kudhibiti miji muhimu na kupata mafanikio kwenye maeneo mengine katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika hapo jana, ushindi ambao tayari rais Recep Tayyip Erdogan, amekiri chama chake kufanya vibaya.

Rais Erdogan hata hivyo ameahidi kuendelea na agenda za kujenga uchumi wa taifa hilo.
Rais Erdogan hata hivyo ameahidi kuendelea na agenda za kujenga uchumi wa taifa hilo. AP - Emrah Gurel
Matangazo ya kibiashara

Huku zaidi ya asilimia 90% ya kura zikiwa zimehesabiwa, Meya wa Istanbul Ekrem Imamoglu, alikuwa akiongoza katika mji mkuu wa Uturuki na kitovu cha kiuchumi, kulingana na Shirika la habari la Serikali.

Kwa ujumla, CHP ilishinda manispaa za majimbo 36 kati ya 81 ya Uturuki, na kufanikiwa kuchukua ngome muhimu za chama cha rais Erdogan, kikipata asilimia 37 ya kura zote ukilinganisha na asilimia 36 za chama tawala, ikiashiria ushindi mkubwa zaidi kwa upinzani tangu Erdogan aingie madarakani miongo miwili iliyopita.

Kwa upande wake rais Erdogan alikiri kushindwa katika hotuba kwa wafuasi wake, akisema chama chake kimepoteza mwelekeo nchi nzima, akidai kuwa raia wametuma ujumbe.

Hata hivyo licha ya kupoteza viti vingi katika uchaguzi ambao ulikuwa kipimo cha ushawishi wake, Rais Erdogan ameahidi kuendelea na agenda za kujenga uchumi wa taifa hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.